Access to Care
Kupata huduma Stahiki
Comfort
Kupewa Faraja Wakati Wote
Privacy
Kutibiwa Katika Faragha
Choice
Kuchagua/Kukataa Huduma Au Mtoa Huduma
Dignity
Kuhudumiwa Kwa Staha/Utu
Safety
Kuhakikishiwa Usalama
Continuity
Kupatiwaa Huduma Endelevu
Information
Kupewa Taarifa Za Matibabu na Gharama
Confidentiality
Kutunziwa Siri za Matibabu na Taarifa Zako
Opinion
Kutoa/Kupokea Maoni na Kusikilizwa
Kufanya Kazi kwa Uhuru bila kuingiliwa na mgonjwa au ndugu wa mgonjwa.
Kujadiliana na jopo la wataalam wenzake kitaaluma kuhusu mgonjwa bila kutoa siri za mgonjwa.
Kutokuwajibishwa kutokana na huduma iliyotolewa kumpa madhara mgonjwa endapo huduma hiyo itakuwa imetolewa kufuatana na utaratibu na miongozo husika.
Kutokutoa huduma kwa mgonjwa endapo mgonjwa ana wasiwasi au ana hisi jambo lolote lisilo la kawaida.
Kuheshimiwa na Mteja.
Kufanya tafiti mbalimbali na kuzisambaza bila kuingilia siri za mgonjwa.
Kutumia mgonjwa kuelekeza wataalam walioko katika mafunzo kwa vitendo.
TOA UPENDO, POKEA UPENDO”
Uongozi wa Hospitali na watoa huduma wote tunakuhakikishia ya kuwa uko katika mikono salama ya watoa huduma mahiri, wenye kuzingatia miongozo, miiko, maadili ya Taaluma zao, taratibu na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Huduma bora zinatolewa kwa usawa na haki kwa watu wote bila kujali dini, wadhifa, kabila au rangi.
Hata hivyo wazee, watoto wadogo, wajawazito na wenye mahitaji maalum ni wajibu wetu sote kuwapa kipaumbele maeneo yote ya huduma.
Mazingira yetu ni salama kwako na kwa watoa huduma, hivyo silaha aina zote sharti zikabidhiwe idara ya ulinzi kabla ya kuingia mazingira ya hospitali.
Tuna kataa kwa nguvu zote lugha za matusi, matendo yasio na staha, vurugu, kudai au kutoa rushwa na mengineyo yanayofanana na haya.
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga utaratibu wa huduma.
“TOA UPENDO, POKEA UPENDO”